24 Agosti 2016 - 21:49
 Korea kaskazini yarusha kombora  lingine

: Korea kaskazini leo imefanikiwa kufanya jaribio la kombora kutoka katika meli ya kijeshi. kombora hilo liliangukia katika bahari ya Japan.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Korea kaskazini  leo imefanikiwa kufanya  jaribio  la kombora  kutoka  katika  meli  ya  kijeshi. kombora  hilo liliangukia  katika  bahari  ya  Japan.

Ni jaribio  la  hivi  karibuni  kabisa miongoni  mwa  majaribio kadhaa yaliyofanywa  na  nchi  hiyo ikikaidi  maazimio ya baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa. Waziri wa mambo  ya  kigeni  wa  Japan  Fumio Kishida amesema jumuiya  ya  kimataifa  inapaswa  kuchukua  hatua.

Jaribio  hilo lilifanyika  siku  mbili  tu  baada  ya  Korea kusini  na  Marekani  kuanza  luteka  yao  ya  kijeshi  ya kila  mwaka  nchini  Korea  kusini, ambayo  Korea  ya kaskazini  inashutumu hatua hiyo.

Marekani imekuwa ikitumia ushawishi wake kuikandamiza nchi hiyo iliyopinga kabisa kuwa chini ya amri za Marekani .

Mwisho wa habari/ 291